Waumini nchini Malawi wamekusanyika katika Shule ya Al-Hadi chini ya uwakilishi wa Al-Mustafa kufanya Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kumuombea Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

7 Julai 2026 - 16:29

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Waumini nchini Malawi wamefanya Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kumuombea Shahidi Sayyid Ali Khamenei Mwenyezi Mungu Amrehemu.

Hafla hiyo imefanyika baada ya Sala ya Adhuhuri na Alasiri katika Msikiti wa Hawzah ya Al-Hadi(as), chini ya uwakilishi wa Al-Mustafa nchini Malawi, ambapo waumini na wapenzi wa marehemu walikusanyika kusoma Qur'ani na kumwombea rehema na daraja za juu mbele ya Mwenyezi Mungu.

Washiriki walisisitiza umuhimu wa kuendeleza maadili, umoja na misingi ya Kiislamu iliyokuwa ikihimizwa na Shahidi Sayyid Ali Khamenei.

Your Comment

You are replying to: .
captcha